SIKU ya Jumatatu klabu ya Stand United ya Shinyanga iliungana na klabu nyingine kubwa nchini katika orodha ya timu zinazonolewa na makocha wa kigeni hususani wanaotoka Ulaya.
Klabu hiyo ambayo hivi karibuni ililamba mkataba mnono kutoka kampuni ya migodi ya dhahabu ya Acacia, ilimsainisha mkataba wa miaka miwili kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig.
Kocha huyo anayetokea Ufaransa ametua Stand na anachukua nafasi ya Mganda Martin Lule aliyekuwa akiinoa timu hiyo iliyoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu uliopita.
Stand inaungana na Simba, Yanga, Azam na pengine Majimaji kama mambo yataenda walivyopanga wanaotaka kumleta kocha kutoka Uingereza kunolewa na makocha wa Ulaya. Mbali na makocha wa Kizungu, pia klabu nyingine kadhaa zimekuwa zikinolewa na makocha wa kigeni kutoka mataifa ya Kenya na Uganda kwa muda mrefu kama ambavyo Coastal Union sasa ipo mikononi mwa Mganda Jackson Mayanja aliyekuwa akiinoa Kagera Sugar.
Ujio wa makocha wa kigeni kwa soka la Tanzania ni jambo zuri ambalo linaoonyesha namna gani soka letu linavyobadilika kila uchao.
Makocha waliopo kwa sasa Tanzania kutoka nje ya nchi siyo wa kwanza, kwani kwa miaka mingi iliyopita Tanzania imekuwa ikishuhudia ujio wa makocha wa aina hiyo.
Hata hivyo kadri miaka inavyosonga mbele, kasi ya ujio wa makocha wa kigeni na hata wachezaji wanaotoka nje imekuwa ukiongeza maradufu siku baada ya siku. Kunaweza kuwa na tafsiri mbili tofauti katika ujio huo wa wageni hao. Ama ni kwamba soka la Tanzania lipo juu kiasi cha kuwavutia wageni hao, ama wameigeuza Tanzania Shamba la Bibi. Shamba wanaloweza kuja kuvuna fedha kisha kujiondokea zao kilaini.
Lakini kwa kuwa Tanzania ni sehemu ya dunia na dunia ya sasa ni kama kijiji, hakuna budi kukubali ujio wa makocha au wachezaji hao, kitu cha muhimu ni kutaka tu kuona wageni hao wanakuwa chachu ya mafanikio kwa klabu zetu na hata timu za taifa.
Mwanaspoti linaamini mamilioni yanayovunwa na makocha na wachezaji hao wa kigeni ni lazima yatoe matokeo chanya yatakayolipeleka mbele soka la Tanzania.
Kwa mfano klabu zenye kumiliki makocha au wachezaji hao na ambazo zinashiriki michuano ya kimataifa ni lazima zijitofautishe na klabu nyingine. Hazipaswi kuendelea kuwa katika muonekano na muendeleo ule ule wa matokeo ya kusononesha.
Klabu za Afrika Kaskazini, Afrika Kusini na hata Kongo (DRC) zimekuwa zikijitofautisha na timu zetu kwa mafanikio kutokana na kuwa na wachezaji na makocha wa kigeni ambao huleta tija katika ushiriki wao.
Kama klabu na timu za taifa za mataifa hayo yenye makocha na wachezaji wa kigeni zinafanya vema ni vipi kwa Tanzania isiwezekane au wanaokuja Tanzania ni ‘vimeo’?