Habari Kuu

Mizengwe iliwang’oa Msimbazi

ACHANA na rekodi wanayoishikilia sasa ya kuambulia patupu kwenye Ligi Kuu Bara kwa miaka mitatu sasa huku ikishindwa pia kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa katika muda huo, lakini klabu ya Simba ina wasifu mwingine wa ziada kuhusu nyota wake.
Simba imekuwa na bahati mbaya ya kuachana na wachezaji wake kitatanishi katika mazingira ambayo yamekuwa yakiacha maswali lukuki.
Siasa zimejaa katika klabu hiyo na wakati mwingine wanaoondoka Msimbazi huwa ni sehemu ya wachezaji wanaopaswa kuwapa mafanikio kwa kiwango walichoonyesha siku za nyuma kabla ya kutemeshwa kibarua kimtindo.
Mwanaspoti linakuanikia baadhi ya mastaa waliondoka Msimbazi kitatanishi na kuacha maswali mengi kwa mashabiki, yaani mizengwe imewaondoka katika klabu hiyo huku wakiendelea kuhitajika.
Amissi Tambwe
Ilikuwa rahisi sana viongozi wa Simba kuwajibu mashabiki wao kuwa wameachana na Tambwe kwa sababu alikuwa haendani na mifumo ya kocha wao kipindi hicho ikiwa chini ya Mzambia Patrik Phiri. Ni sawa na viongozi wa kisiasa wanaopenda kutoa majibu mepesi katika maswali magumu. Nani hajui namna Mrundi huyo alivyofanya kazi yake kwa umakini mkubwa Msimbazi alipoichezea msimu wa 2013-2014 na kuifungia mabao 19 katika Ligi Kuu.
Hata hivyo, siasa za soka la Bongo zilimwondosha mkali huyo wa mabao Msimbazi kitatanishi na watani zao Yanga walimnyakua. Kwa kipindi kifupi alichoichezea, Tambwe ameibeba Yanga kwa kuifungia mabao 14 na kusaidia kutwaa ubingwa.
Cha ajabu ni kwamba wachezaji waliosababisha Tambwe atembwe Dan Sserunkuma na Emmanuel Okwi hawakuwa na jipya la kufanya kwani klabu ilimaliza katika nafasi ya tatu na kuendelea kubaki kuwa ‘Wahapahapa’.
Ramadhan Singano ‘Messi’
Hili ni tunda la zao la soka la vijana kwa klabu ya Simba. Singano maarufu kwa jina la Messi aliibukia Simba B na tangu alipopandishwa katika kikosi cha wakubwa, kila kocha aliyepita kuinoa timu hiyo ameweza kumtumia mchezaji huyo katika kikosi chake. Hata hivyo, maajabu yale yale ya siasa za soka zinazozitafuta klabu za Tanzania zilimkumba nyota huyo na kuondoka kilaini kutua Azam hivi karibuni.
Linalowashangaza wadau wa soka pamoja na mashabiki wa Simba na wachezaji wa zamani wa kikosi hicho baada ya kusikia Singano wanaburuzana na viongozi wake TFF, ambaye wamemlea kiwango chake kwa utata wa mkataba na awali pia TFF, walitoa majibu tata.
Kilichoshuhudiwa baadaye ni viongozi wa Simba kugaragazwa na Messi kwa KO ya aibu, huku dogo akienda kula matunda ya kipaji cha soka Azam, huku Msimbazi wakiwa hawaelewi kitu ikizingatiwa kuwa hata ‘roho yao’ Emmanuel Okwi naye keshauzwa Denmark.

Next
This is the most recent post.
Older Post
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
Item Reviewed: Mizengwe iliwang’oa Msimbazi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top